Thursday 11 April 2013

Mama wa watoto walionyongwa afariki


MAMA mzazi wa watoto watatu wanaodaiwa kuuawa kikatili kwa kunyongwa na baba yao mzazi, amefariki dunia.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema jana kuwa mama huyo Jacqueline Luvika (21), ambaye alikuwa kalazwa katika Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mamba tangu Jumamosi iliyopita, amefariki dunia Jumapili jioni alipofikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa matibabu zaidi.
Inadaiwa mwanamke huyo alitumbukizwa kisimani na mumewe kufanya unyama huo, na kwamba alikutwa akiwa amepoteza fahamu.
Baadhi ya ndugu na marafiki wa marehemu wamedai kuwa tayari mwili huo umechukuliwa kwa maziko kijijini Majimoto baada ya kufanyiwa uchunguzi.
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, Jeshi la Polisi bado linamshikilia mtuhumiwa huyo, Justine Albert (24) kwa kuwaua kikatili watoto wake watatu kwa kuwanyonga kisha kuitumbukiza miili yao kwenye kisima cha jirani kijijini humo.
Inadawa mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa na mahusiano ya kimapenzi na jirani yao na kwamba baadhi ya watoto hao amezaa nje ya ndoa yao.
Kidavashari alidai kuwa mtuhumiwa huyo alitenda unyama huo Jumamosi iliyopita, majira ya saa 11:30 alfajiri katika Kijiji cha Majimoto.
Aliwataja watoto wanaodaiwa kunyongwa na baba yao kuwa ni Frank Justine (6), Elizabeth Justine (4) na Maria Justine mwenye umri wa miezi minne.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment