WANAWAKE nchini wametakiwa kutumia kampeni za kutahiri wanaume zinazoendelea nchini kuwahamasisha wanaume zao kwenda kutahiriwa.
Ushauri huo ulitolewa mjini hapa jana na mtaalamu mshauri wa programu za afya na maendeleo (AMCA Interconsalt) na mwezeshaji wa masuala ya ukimwi, Abdallah Mwichande, alipokuwa akitoa elimu kuhusu masuala ya maambukizo ya ukimwi kwa watumishi wa Wizara ya Ushirika na Masoko mkoani hapa.
“Wanawake hakikisheni mnapokutana na wanaume ambao hawajatahiriwa mnawahamasisha kwenda kutahiriwa ili kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi,” alisema.
Alisema wanaume ambao hawajatahiriwa wanachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la maambukizo ya VVU nchini, hivyo kuna kila sababu ya kuhakikisha wanaume ambao hawajatahiriwa wanafanya hivyo mara moja.
Hata hivyo, aliwaasa wanaume hao ambao watatahiriwa kutoona wamepata kinga ya kudumu baada ya zoezi hilo, hivyo kujikuta wakifanya mapenzi yasiyo salama.

chanzo:daima
No comments:
Post a Comment