MAJERUHI mwingine mhanga wa mlipuko wa bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti, Isabela Michael (19), amefariki katika Hospitali ya Mtakatifu Elizabeth.
Taarifa hizo zimepatikana jana hospitalini hapo baada ya ziara iliyofanywa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, na kupewa taarifa hiyo na Mganga Mkuu wa Hospitali ya St. Elizabeth, Goodluck Kwayu.
Kifo cha Isabela ambaye mama yake mzazi naye yuko mahtuti hospitalini hapo, kinafanya idadi ya watu waliokufa kutokana na kurushiwa bomu hilo katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti jijini hapa kufikia wanne.
Katika tukio hilo, zaidi ya watu 66 walijeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, hospitali binafsi ya Selian na St. Elizabeth.
Rais Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Naibu Waziri Nyalandu Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd ni miongoni mwa viongozi waliofika hospitalini na katika familia za marehemu kuwapa pole.
Viongozi hao waliwataka Watanzania kuendelea kuishi kwa umoja, amani na utulivu vilivyodumu kwa muda mrefu sasa badala ya kugawanyika baada ya tukio la mlipuko wa bomu hilo.
“Tukio hili lisitugawe Wakristo na Waislamu, tuna historia ya muda mrefu ya kushirikiana vizuri,” alisema.

chanzo:daima
No comments:
Post a Comment