Monday 17 June 2013

Lwakatare: Nilimwona Mungu nikiwa mahabusu

MKURUGENZI wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare amesema siku 92 alizokaa gerezani, alimwona Mungu, ndiyo maana yupo nje kwa dhamana.
Pamoja na kumwona Mungu, mkurugenzi huyo ameahidi kuandika kitabu kinachoelezea maisha yake hatua kwa hatua jinsi alivyoishi mahabusu kwa siku hizo.
“Nimeamua kutengeneza kitabu kitakachoelezea maisha yangu hatua kwa hatua siku zote 92 nilizokaa mahabusu,” alisema Lwakatare wakati wa ibada ya shukrani kwa Mungu iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Usharika wa King’ong’o, Kimara jijini Dar es Salaam.
Lwakatare alikamatwa Machi 11 mwaka huu na kuachiwa kwa dhamana Juni 11 kwa tuhuma za ugaidi kabla ya kufutwa na kubaki na shitaka la kupanga njama za kutaka kumdhuru Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Denis Msacky
.
Alisema Mungu amejibu maombi yake bila kuangalia dini, dhehebu wala itikadi. “Washarika wenzangu Mungu anajibu maombi kama utamwomba kwa nafsi moja… nikiwa gerezani nimejifunza kitu kimoja, Mungu hakujibu kwa sababu wewe ni dini fulani, dhehebu fulani au chama fuani, anajibu kama utanyenyekea na kupeleka hitaji lako.”
Alisema akiwa gerezani na mahabusu mwenzake Sheikh Ponda Issa Ponda, kila mtu alikuwa akitumia muda wake mwingi kumwomba Mungu kwa imani anayoamini.
chanzo:chadema

No comments:

Post a Comment