Hofu ya ugonjwa wa Ebola imetanda katika mkoa wa Morogoro baada ya raia mmoja wa Malawi mwanaume mwenye umri wa miaka 29 kupelekwa katika hospital ya mkoa huo na polisi huku akitokwa damu sehemu mbalimbali za mwili wake.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Godfrey Mtei, alisema walimpokea mgonjwa huyo Juni 18 mwaka huu majira ya saa 3 asubuhi, akiwa katika hali mbaya ya kutokwa na damu katika sehemu mbalimbali za mwili wake na kuzusha hofu kuwa ni ugonjwa wa Ebola kutokana na dalili kufanana na ugonjwa huo hatari.
Alisema mara baada ya kufikishwa mgonjwa huyo alifanyiwa vipimo mbalimbali na kugundulika kuwa hana ugonjwa wa Ebola kama ambavyo taarifa zilikuwa zimesha enea kuwa ugonjwa ebola umeingia ndani ya mkoa wa Morogoro.
Alisema walipofanya mahojiano na mgonjwa huyo alieleza kuwa ugonjwa wa kutokwa na damu sehemu mbalimbali katika mwili wake unamsumbua kwa miezi mitatu sasa na hutibiwa na kuendelea na shughuli zake kama kawaida.
Aliwataka wananchi wa mkoa huo wasiwe na wasiwasi kuhusu mgonjwa huyo, kwani wamejiridhisha sio ugonjwa wa Ebola na hiyo wasiogope kwenda kupata huduma katika hospitali hiyo wakihofia kuambukizwa.
chanzo:nipashe
No comments:
Post a Comment