kauli ya Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy (CCM), akitahadharisha kwamba ipo siku Tanzania itaongozwa na rais anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja ‘shoga’.
Kwa mujibu wa habari hiyo, Keissy alitoa tahadhari hiyo mjini Dodoma wakati wa mkutano wa siku tatu wa Chama cha Wabunge Wanaopambana na Ukimwi.
“Mnashindwa kuwalea watoto wenu mnawapeleka shule za bweni wakiwa na miaka mitatu ili walelewe Kizungu, huko watapakwa mafuta ya KY na wataingiliwa,” sehemu ya habari hiyo ilimnukuu Keissy.
Mbunge huyo alitoa mfano wa mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo mashoga zaidi ya 400 walihudhuria mkutano huo huku akisisitiza kwamba bila serikali kuchukua hatua za kupiga marufuku nchi itaelekea pabaya.
Mbunge huyo alikuwa akiikumbusha jamii hususan wazazi na walezi ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao kwa sababu za utandawazi na maendeleo yaliyopo duniani.
Tunaunga mkono kauli ya mbunge huyo kwa sababu zifuatazo, uwepo wa mitandao ya kijamii na mifarakano ndani ya familia ni kichocheo cha mmomonyoko wa maadili mema.
Tunaamini kwamba familia zenye amani na utulivu zina uwezo wa kufuatilia nyendo za watoto wao na kuwaonya pale wanapokwenda kinyume cha maadili.
Hivi sasa ule ushirikiano katika malezi uliokuwepo miaka 10 na zaidi iliyopita hivi sasa haupo, badala yake kila mzazi anamwona mtoto wake ni bora zaidi ya mwingine.
Ni kitu cha kawaida kwa siku za hivi karibuni kumwona kijana akishindwa hata kumsalimia mtu aliyemzidi umri, ule utaratibu wa kuwapokea mizigo na kuwasindikiza hadi nyumbani umebaki stori.
Kibaya zaidi, hata kwenye daladala ni nadra kumkuta kijana anampisha kiti mtu mzima, mjamzito au mama aliyebeba mtoto, taifa limetawaliwa na ubinafsi, upendo umetoweka.
Siku hizi watu wazima, wake kwa waume ndio wanaoongoza kuwarubuni vijana ambao wengi wao wamegubikwa na tamaa ya fedha.
Hali ni mbaya zaidi kwenye vyuo vyetu vya elimu ya juu, ambako taifa linategemea kupata wasomi wa kada mbalimbali watakaoiongoza nchi, lakini ndiko kwenye hali mbaya, kwa sababu sodoma na gomora imeshamiri.
Tumesikia na kuona kwenye mitandao ya kijamii wanavyuo hao wakifanya matendo hayo ambayo ni chukizo mbele ya Mungu na wanadamu.
Vijana wanaharibika, maadili mema yanazidi kupotea, wavulana wanafanya mambo ya kike na mavazi yao ni nusu utupu. Wasichana nao wanasagana, nani wa kumkosoa mwingine?
Tunaishauri serikali kuanza utekelezaji wa sheria zilizopo ili kudhibiti matendo haya, vinginevyo mambo ya kisasa tunayoletewa kutoka nchi za Magharibi yanatupeleka pabaya.
Tunaamini sheria zinazozuia mapenzi ya jinsia moja zipo ila tunatakiwa kuziboresha kwa kuweka adhabu kali kwa wahusika.
Chanzo:daima
No comments:
Post a Comment