Monday, 22 July 2013

DK. CHENI AMTOA CHOZI LULU

MWIGIZAJI the big name wa filamu za Kibongo, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, Alhamisi iliyopita, Julai 18, mwaka huu ilikuwa siku yake ya kuzaliwa ‘birthday’ iliyomfanya staa mwenzake, Elizabeth Michael kutokwa chozi.
Kama kawaida kwa siku muhimu kama hiyo kwa kila mtu, watu mbalimbali humtakia mhusika afya njema, maisha marefu, mafanikio na kila la heri huku wengine pia wakitoa au kuelezea hisia zao kwa mlengwa. 
Katika hilo, Lulu aliamua kumtakia Dk. Cheni heri ya siku ya kuzaliwa kwa kumuelezea kuwa ni mtu muhimu katika maisha yake kwa kuwa na upendo wa dhati kwake na kumthamini hivyo alitumia siku hiyo kumtafakari hadi akatokwa na machozi. 
“Daah! Hata sijui nianzie wapi…oke... amekuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yangu...mtu mwenye kunipenda kwa dhati na kunithamini...kila ninapokuwa najaribu kumuelezea huwa nakosa cha kuongea na naishia kulia tu..! 
“Nina uhakika sina cha kumlipa zaidi ya kumuombea aishi maisha marefu yenye amani, afya na faraja! Happy Birthday Daddy Cheni...” aliandika Lulu kwenye ukurasa wake katika mtandao wa Instagram.
Dk. Cheni ndiye aliyemuingiza Lulu katika sanaa kwa kumpeleka Kaole Sanaa Group na hata baada ya kukumbwa na matatizo wakati wa kifo cha Steven Kanumba, bado yupo naye bega kwa bega. 
Dk. Cheni ni mmoja wa waigizaji wenye mchango mkubwa katika tasnia ya maigizo na filamu Bongo ambaye alitamba na michezo kadhaa kipindi hicho ITV na baadaye katika filamu na kusababisha waigizaji wengi chipukizi kuhamasika kuingia katika sanaa ya filamu. 
Baadhi ya filamu alizoigiza ni pamoja na Nipende Monalisa, Danger Zone, Majanga, Jessica na nyinginezo.
chanzo:.globalpublishers

No comments:

Post a Comment