Kwa kifupi , yupo kijana mmoja mtu wangu wa karibu alinijia kunitaka ushauri, akaanza kwa kuiniambia kuwa huyu anayemlalamikia ni mama yake mdogo mzaliwa na mama yao ambaye alishafariki muda mrefu, kiasi yeye anamchukulia kama ndiye mama mzazi.
Anasema, katika familia yao, ndugu zake Mungu amewajalia nafuu ya maisha. Wapo wenye nyumba, magari na kadhalika. Ila yeye Mungu bado hajamfungulia hali kama nduguze.
Bado anaishi nyumba ya kupanga. Anasema mara nyingi mama yao huyu anapokuja Dar anawatembelea ndugu zake wote kasoro yeye tu na hajawahi kumkosea kosa lolote.
Anasema hali hiyo inamfanya ajisikie mnyonge sana kiasi anafikiria hali hiyo inasababishwa na utofauti wa kipato alicho nacho na nduguze(hapa alianza kutokwa na machozi). Nikamnyamazisha nikamwambia awe na subira kwani Mungu ndiye mgawaji wa yote.
Mwisho, wangu sikupenda jambo hilo nilifahamu peke yangu nimeona nililete katika safu hii ya Maisha Ndivyo yalivyo kwa maoni na ushauri.
No comments:
Post a Comment