Thursday, 25 July 2013

Mtoto akamatwa na ngozi za chui zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 22.8

Jeshi la Polisi mkoani Tanga linamshikia mtoto mwenye umri wa miaka 17 kwa tuhuma za kukutwa na ngozi nne za chui zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 22.8

Kwa mujibu wa Kamanda wake, Constantine Massawe mtoto huyo Mkazi wa Wilaya ya Handeni, alikamatwa kati ya Julai 21 na 23 mwaka huu wakati wa msako wa polisi uliofanywa kwa kushirikiana na Maafisa Wanyama Pori.

Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa  nyumbani kwao katika eneo la Zizini akiwa na ngozi hizo.
Vilevile alisema walimkamata Iddi Chamola(47) na ngozi mbili za chui zenye thamani ya Sh. milioni 11.4.

Alisema mtuhumiwa huyo  alikamatwa katika eneo la nyumba ya  wageni iitwayo Makoko akiwa na ngozi hizo.

“Operesheni hii ni kwa ajili ya kutafuta wahujumu wa nyara za serikali ... watambue kuwa itakuwa endelevu na tutawatia mbaroni wahusika wote," alisisitiza.

 Alisema watuhumiwa hao  wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
chanzo:nipashe
 

No comments:

Post a Comment