Monday, 22 July 2013

Polisi yagawa kondomu kwa `machangudoa`

Kufuatia kutokuwepo kwa sheria ya kuwashitaki machangudoa na kaka poa, jeshi la polisi limeanza kampeni ya kugawa kondomu kwa watu hao ili kuwakinga na magonjwa ya ngono na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU).
Jeshi hilo limesema linawakamata machangudoa na kaka poa lakini wanapofikishwa mahakamani wanapewa adhabu ndogo ikiwa ni pamoja na vifungo vya muda mfupi na kurudi tena kuendelea na kazi yao hali inayovunja moyo jeshi hilo.
kutokana na hali hiyo jeshi lake limeamua kuchukua hatua hiyo ya kutoa kondomu ili wasiendelee kusambaza magonjwa yanayosababishwa na ngono.
Mwanasheria wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), Pecience Mlowe, alisema serikali inatakiwa iandae sheria ya kuwashitaki machangudoa, na kuongeza kuwa mahakama kwa sasa inatumia sheria ya uzururaji na ya kuendesha madanguro kwa ajili ya kuwaadhibu watu hao.
Mlowe alifafanua kuwa sheria zinazotumiwa na mahakama ni zile zilizorithiwa kwa wakoloni ambazo haziendani na mazingira ya sasa, pia sheria zilizopo hazijafafanua kuwa changudoa au kaka poa anaonekanaje, maeneo gani, kama ilivyo sheria ya wizi inafafanua kuwa mtu akitoa kitu na kukiweka sehemu nyingine anachukuliwa kuwa ni wizi.
Naye mmoja wa wasichana anayefanya biashara ya kuuza mwili aliyejitaja kwa jina moja la Halima, alisema polisi wanapowakamata, mara nyingine wanawadhalilisha kwa kuwalazimisha kufanya nao mapenzi.
chanzo:nipashe

No comments:

Post a Comment