Swali la wiki hii liliuliza:
Utakuta mwanamke anapekua simu ya mumewe au mwanaume anapekua ya mkewe, pengine msichana anapekua simu ya mpenzi wake au mvulana anafanya hivyo. Kupekuliana simu ni sawa?
Wadau wa safu hii walijibu hivi:
Prosper Mallya, Moshi
Suala la kupekua simu ya mke wako au mume wako, mie naona ni suala ambalo limeshakua kama ni mazoea, maana nyingine ni kama ngozi yako ya mwili hapo ni uaminifu tu unahitajika.
Danny Chumu, Dar es Salaam
Kupekua pekua simu ya mpenzi wako siyo jambo jema hata kidogo inafaa kuaminiana tu wala sioni haja ya kupekua katika simu ya mwenzi wako.
Ashura Amily, Kibaha
Kupekua simu ya mkeo/mumeo au mpenzi wako ni sawa hapo ndiyo mtaaminiana na mapenzi mliyokuwa nayo ni ya kweli unapata kujua tabia za mwenzi wako.
Elias Ndeki, Arusha
Kiukweli siyo busara kupekualiana simu, kwani inaonyesha ni jinsi gani hamwaminiani kimaisha na mwenzi
Kaoneka FJ, Mbarali
Kupekualiana simu ni sawa na pengine mfumo wa simu mnazotumia ni tofauti, kujihami na simu kutamtia hofu mwenza wako, atahisi wewe si mwaminifu.
Festo Lukoo, Morogoro
Suala la kupekua simu ya mkeo au mumeo siyo ustaarabu unaweza kujipa presha wenye tabia hiyo waache.
Lucius Hindi, Songea
Ni sahihi kupekuliana simu lakini usikurupuke kufanya hivyo.
Omar Ferouz, Morogoro
Kupekualiana simu kwa wapenzi si jambo sahihi kabisa, kwani inaweza kusababisha kuachana kwa jambo dogo kabisa ambalo umekutana nalo kwenye simu ya mwenzi wako.
William Mekson, Kimara Dar
Nikutojiamini au kuaminiana sidhani kama kuna haja ya kupekua simu ya mwenzako, wakati kila mtu ana simu yake sanasana kujipa presha.
Kitikiro Zacharia, Moshi
Kupekualiana simu siyo sawa na ndiyo mwanzo wa kutoelewana na kutoaminiana kikubwa ni kila mmoja kutoshika simu ya mwenzake
Kupekua simu ya mwenzi wako si sahihi kuna vitu ni vya kibinafsi zaidi na haviwezi kuwa vya kushirikiana hata kama mpo kwenye ndoa, ni vyema watu wakaheshimu faragha za wenza wao ikiwa pamoja na simu.
No comments:
Post a Comment