Monday, 9 September 2013

Bilionea wa Afrika awekeza sekta ya madini Kenya

Nairobi. Miongoni mwa mabilionea wakubwa  Afrika ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa Nigeria, Aliko Dangote amesema atawekeza dola za kimarekani milioni 400 katika sekta ya madini nchini Kenya.
Dangote ambaye aliwasili Kenya wiki iliyopita pamoja na  Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria, alisema yuko tayari kuwekeza katika sekta ya madini ya Kenya ili kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.
Waziri wa madini wa Kenya, Najib Balala alipongeza hatua hiyo ya Dangote na kufurahia ushirikiano wake na tume iliyoundwa na Serikali ya Kenya ya kuchunguza utaratibu wa utoaji leseni za kuwekeza katika sekta ya madini nchini Kenya. Balala  alitumia pia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wengine katika sekta hiyo ya Madini,ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi.
“Namshukuru sana Dangote kwa kukubali kuwekeza katika sekta hii ya madini hapa Kenya kwani atatusaidia kukuza uchumi wa nchi yetu, pia natumia fursa hii kuwakaribisha wengine,’’ alisema  Balala.
Awali Kenya ilisema kwamba  itafuata moja kwa moja sera na mfumo wa udhibiti wa madini kama unaotumiwa na Tanzania kwa sababu mageuzi yaliyofanywana Serikali katika sekta ya madini ni dhahiri kuwa yameanza kuzaa matunda.
Kenya iliiwashauri Watanzania kuwa  ni vyema kupata Katiba Mpya, lakini Katiba peke yake haiwezi kuleta maendeleoya wananchi kwani maendeleo yataletwa na juhudi za wananchi wenyewe.
Hayo yalisemwa na Balozi wa Kenya nchini,  Mutinda Mutiso alipokuwa akimuaga  Rais Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.
chanzo:mwananchi


No comments:

Post a Comment