MSANII mahiri wa Bongo Fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’ ameingia mkataba wa kibiashara na Kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘My Number One’.
Kibao hicho kitatumika kama mwito kwa mpigaji wa simu ‘caller tone’, ambapo mteja wa Vodacom atapata nafasi ya kujishindia sh 50,000 pale atakapoutumia wimbo huo.
Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, msanii huyo anayebamba katika ‘game’ hivi sasa hapa nchini na Afrika Mashariki, alisema kuwa wakati umefika kwa wao kuongeza ubunifu ili kampuni kubwa ziweze kutumia nyimbo zao kibiashara ili kuwaongezea mapato.
Kwa upande wake, Mkuu wa Masoko na Udhamini wa Vodacom, Kelvin Twissa, alisema kuwa hatua hiyo itasababisha kupatikana kwa washindi watano kila siku, pia mbali ya wimbo huo wa’ My Number One’ wa Diamond, ambao ndio unaobamba katika anga la muziki hivi sasa, lakini pia hata nyimbo za wasanii wengine pia zitampatia mteja fursa ya kushinda.
“Ili kuchagua mwito huo na mingine, wateja wanashauriwa kupiga simu kwenye mtandao wa Vodacom kupitia namba 15577 au kubonyeza nyota na kuweza kupata wimbo huo,” alifafanua Twissa.
chanzo:daima
No comments:
Post a Comment