Hamkani Zanzibar si shwari tena! Ile hali ya amani na utulivu katika visiwa hivi vyenye utajiri mkubwa wa vivutio vya utalii haipo tena kama zamani. Imetetereka.
Habari kubwa katika maeneo mengi ya Zanzibar, hasa Unguja mjini ni juu ya janga litokanalo na kimiminika cha tindikali.
Watu wanamwagiwa tindikali. Kasi ya kunaswa kwa wahalifu wanaoendesha operesheni hiyo ya kinyama bado inaonekana kuwa ndogo na hivyo mizizi ya hofu kuendelea kujikita nyoyoni mwa wananchi walio wengi.
Wapo wanaolia baada ya kuguswa moja kwa moja na balaa hili la kumwagiwa tindikali. Wapo wanaobubujikwa machozi kila uchao kutokana na madhara makubwa yaliyowapata wapendwa wao.
Kuna kundi kubwa pia la wanawake na watoto waliofutiwa baadhi ya ndoto zao nyingi kimaisha baada ya watu waliokuwa wakiwategemea kufanikisha malengo yao kukumbwa na balaa hili.
Maeneo kama Mji Mkongwe (Stone Town) wanazungumzia tindikali, Malindi wanajadili tindikali, Mwanakwerekwe, Mnazi Mmoja, Jang'ombe, Raha Leo, Mchambawima, Fuoni, Tunguu, Amaan na watu wa maeneo mengine mengi tu ya Zanzibar hawako nyuma katika kujadili hili na lile kuhusiana na kuongezeka ghafla kwa aina hii ya uhalifu wa kizazi cha sasa.
Ndiyo. Nani asiache kujadili kemikali hii iliyo katika hali ya kimiminika visiwani Zanzibar?
Na kwanini wasijadili ilhali hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa matukio mengi ya watu wasiokuwa na hatia kumwagiwa tindikali kwa sababu zisizofahamika wazi?
Hadi sasa, tayari kuna orodha ya matukio kadhaa ya kuogofya kuhusiana na mashambulizi ya aina hiyo ya kemikali; ambayo sifa yake kubwa ni kumuunguza vibaya mtu anayemwagiwa, kumuachia maumivu makali yatokanayo na majeraha makubwa, kumbadili mtu haiba yake daima milele kwa namna ya kusikitisha na pia kuwapofusha wale wanaoingiwa machoni na kimiminika hicho cha aina tofauti kamaSulphuric Acid, Hydrochloric Acid na Nitric Acid.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, anasema kuwa kwa muongo mmoja sasa, tayari kuna matukio takriban saba yanayohusiana na watu kuletewa madhara makubwa baada ya kumwagiwa tindikali.
Anakiri kwamba matukio hayo, mengi yamejiri katika miaka ya hivi karibuni; hivyo kuzua hofu kubwa kwa wakazi wa visiwa hivyo.
Miongoni mwa wale wanaotajwa na Kamishna Mussa ni mwananchi aitwaye Masoud Mohamed Shambi, mkazi wa kisiwa cha Pemba. Alikumbwa na mkasa huu mwaka 2000. Huyu alikuwa amelala chumbani kwake.
Ghafla, katikati ya usiku wa manane, akajiwa na mtu asiyejulikana ambaye alimrushia tindikali kutokea dirishani.
Tukio hilo lilihusishwa na vuguvugu kali la siasa wakati huo baina ya vyama viwili hasimu visiwani hapa; Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Zanzibar, Rashid Ali Juma (45), aliunganishwa katika orodha ya waathirika wa tindikali baada ya kumwagiwa na mtu asiyejulikana na kudhuriwa kwa takriban asilimia 25 ya mwili wake.
Tukio hili lilitokea Februari 18, 2011, saa 2:30 usiku, nje ya Msikiti wa Amaan ambako Rashid alikuwa amekaa baada ya kumaliza ibada ya swala ya isha.
Wengi walilihusisha tukio hili na utekelezaji wa majukumu ya kazi ya Rashid, hasa baada ya mtumishi huyo wa umma kusimamia operesheni kadhaa zilizomfanya azozane na baadhi ya wafanyabiashara wa makontena eneo la Darajani waliokuwa wakipinga mpango uliokuwa ukisimamiwa naye wa kuwaondoa ili kupisha ujenzi wa maegesho ya magari na bustani.
Novemba 5, 2012, Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga, alikumbwa pia na mkasa huu baada ya kumwagiwa tindikali na mtu asiyefahamika wakati akifanya mazoezi ya viungo kwenye Uwanja wa Mwanakwerekwe.
Tukio hilo lilijiri alfajiri ya Jumanne, ikiwa ni siku tatu tu baada ya mwanazuoni huyo wa Kiislamu kutoa hotuba ya kulaani vurugu wakati wa swala ya Ijumaa kwenye msikiti anaouongoza wa Mwembe Shauri na kuwataka wananchi wa Zanzibar wajiepushe na vitendo vya aina hiyo kwani madhara yake ni makubwa kwa jamii.
Sheikh huyu aliumizwa vibaya, akiathirika kuanzia usoni, kifuani, tumboni, ubavuni na hata mapajani. Hadi sasa, haijajulikana hasa nini chanzo cha shambulizi hilo na pia, ni nani walikuwa nyuma ya uovu huo.
Tukio jingine la tindikali Zanzibar lilitokea mwaka 2012 na kumhusisha mfanyabiashara mwenye asili ya Kiasia, Chandurali Chunilai Asawala.
Kwa mujibu wa Kamishna Mussa, huyu ni mmiliki wa stoo ya pombe na kwamba alimwagiwa tindikali katika tukio la uporaji wakati yeye na mkewe wakisafirisha fedha.
Alimwagiwa na watu waliomvamia akiwa njiani, akaporwa Sh. 700,000 na kuachwa akiwa na majeraha tele mwilini.
Mei 23, 2013, Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mohamed Said Omar, maarufu kwa jina la Kidevu, alikumbwa pia na mkasa huu wa kutisha wa kumwagiwa tindikali.
Tukio hili lilijiri mishale ya saa 2:00 usiku. Hadi sasa haijafahamika hasa ni nani aliyehusika na kwa nini aliamua kufanya unyama huo dhidi ya kiongozi wa serikali.
Hata hivyo, wapo wanaohusishwa katika tukio hilo na kadhia ya maandalizi ya daftari la wakazi wa shehia hiyo kwani viongozi walikuwa wakihakikisha kuwa kila mwananchi wa Zanzibar ni lazima awe ameishi katika shehia husika kwa miaka mitatu ndipo aandikishwe.
Baadhi ya wananchi hawakuwa wakikidhi kigezo hicho muhimu na hivyo kukumbana na ugumu ambao unatajwa kuwa chanzo kimojawapo cha mgogoro.
Agosti 7, 2013, mishale ya saa 1:15 usiku, watu wawili waliokuwa katika pikipiki kwenye eneo la Mji Mkongwe, Mtaa wa Shangani, waliwamwagia tindikali mabinti wawili, raia wa Uingereza Katie Gee (18) na Kirstie Trup (18) waliokuwa Zanzibar wakifanya kazi ya ualimu kwa kujitolea. Ilibainika kuwa kimiminika hicho kilikuwa ni aina ya sulphuric acid. Chanzo cha shambulizi hili na wahusika wake pia bado ni utata.
Kamishna Mussa anasema kuwa tayari kuna watu watatu wanashikiliwa kuhusiana na tukio hili na upelelezi wake ulishakamilika na jalada kufikishwa katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Ibrahim Mzee Ibrahim.
Wiki moja tu iliyopita (Septemba 14, 2013), unyama utokanao na mashambulizi ya tindikali visiwani Zanzibar ukamkuta Padri Ancelmo Mwang'amba wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Cheju.
Huyu alimwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana katika maeneo ya Mlandege, wakati akitoka kwenye kituo cha kutolea huduma za intaneti kiitwacho Sun Shine.
Kiongozi huyu wa kiroho ameunguzwa vibaya. Muonekano wake sasa ni wa kusikitisha mno. Amejeruhiwa sana usoni, kifuani, mikononi, sehemu ya tumbo na maeneo mengine mwilini.
Alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi baada ya kupatiwa huduma katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Wiki iliyopita, Padri Mwang'amba alipelekwa India kwa matibabu zaidi.
Kama ilivyokuwa kwa matukio mengine mengi, hili nalo bado halijajulikana chanzo chake na Kamishna Mussa anasema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi.
Ikumbukwe kuwa wakati wa vuguvugu la uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, Katibu Msaidizi Mkuu wa CCM, Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar, Ali Mwinyi Msuko, aliwahi pia kukumbwa na kadhia ya kumwagiwa tindikali.
Tukio hilo lilijiri Pemba, eneo la Mtemani Maghorofani, mishale ya saa 2:00 usiku. Mtu asiyejulikana alimmwagia tindikali Msuko na kumuunguza vibaya kifuani na maeneo ya tumboni.
Mtu mmoja alikamatwa na baadaye kuachiwa huru kuhusiana na tukio hilo.
Wakati hali ikiendelea kuwa tete kutokana na mfululizo wa matukio ya kumwagiana tindikali visiwani Zanzibar, wananchi wa Tanzania Bara pia hawajasalimika sana.
Yapo matukio kadhaa pia ya unyama utokanao na mashambulizi ya tindikali.
Mwaka 1995, aliyewahi kuwa Mbunge wa Mwanza Mjini, Said Shomari alimwagiwa tindikali na kujeruhiwa vibaya mwilini, hasa sehemu za shingoni.
Shomari alikumbwa na kadhia hii akiwa ofisini kwake jijini Mwanza. Mwaka huo huo, mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) aitwaye Kombe pia alikumbwa na tukio la kumwagiwa tindikali jijini Mwanza, sawa na kadhia iliyomkuta Diwani wa Kata ya Kitangiri jijini humo, Sylivester Lubala.
Usiku wa kuamkia Julai 13, Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba alikumbwa pia na tukio la kumwagiwa tindikali wakati akiwa nyumbani kwake eneo la Kwamrombo, Arusha.
Shekhe Makamba ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Sekei mjini Arusha, alikumbwa na tukio hilo baada ya kumaliza kuswali swala ya taraweh (huswaliwa usiku wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani).
Hakikufahamika chanzo wala wahusika wakuu wa tukio hilo.
Mwingine aliyekumbwa na tukio hilo ni mmiliki wa maduka ya Home Shopping Centre, Said Mohamed Saad. Yeye alimwagiwa tindikali Julai 19, 2013, saa 2:00 usiku wakati akiwa kwenye jengo kubwa la biashara la Msasani City Mall.
Hadi sasa, Saad aliyeunguzwa vibaya usoni, yuko nje ya nchi akiendelea kutibiwa. Mtu aliyemfanyia unyama huo anadaiwa kuwa alifanikiwa kutoroka kwa pikipiki aliyofika nayo kwenye eneo la tukio.
KWANINI TINDIKALI?
Kamishna Mussa anasema wanaowamwagia watu tindikali Zanzibar ni wahalifu kama wengine wote, wenye nia mbaya ya kujeruhi na hata kuua.
Kwamba, kwa sababu zozote zile; iwe ni za kisiasa, kibiashara, imani kali za kidini, uporaji na nyinginezo, bado inaonekana wazi kwamba washambuliaji huwa na nia mbaya ya kudhuru na tindikali inaonekana kuwa ndiyo silaha rahisi kwao kuipata. Anasema kuwa ni dhahiri, wahalifu hawa wanaotumia tindikali kudhuru wengine wangeweza pia kutumia hata risasi kama wangepata mwanya wa kumiliki bastola na bunduki.
"Ni wazi kwamba si rahisi kupata silaha kama bastola hapa Zanzibar... lakini tindikali imeenea, kuna vibali vya biashara hii vimekuwa vikitolewa na manispaa. Lakini kwa ujumla udhibiti wake si mzuri sana... na ndipo wahalifu wanapoitumia kemikali hii kama silaha," anasema Kamishna Mussa.
"Na sasa tumeanza harakati za kukutana na wadau wote ili kuona ni namna gani tutazuia upatikanaji holela wa tindikali... na kuanzia Septemba 14 (2013) tumeanza operesheni maalum ya kusaka tindikali. Tumeshakamata zaidi ya lita 30 za tindikali mbalimbali kama za Nitric na Sulphuric,"
Mkemia Mkuu wa Zanzibar, Slim Rashid Juma, anasema kuwa tindikali iko katika kundi la kemikali hatari zinazohitaji kutumiwa kwa uangalifu mkubwa.

Hata hivyo, anasema kwa bahati mbaya hadi sasa hakuna kanuni imara na ofisi yake ikishirikiana na mamlaka nyingine za serikali iko katika mchakato wa kuandaa kanuni zitakazosaidia kudhibiti kemikali hatari visiwani humo.
"Kwa namna taratibu za uandaaji sheria na kanuni zilivyo, zoezi hili linaweza kukamilika ndani ya mwaka mmoja. Baada ya hapo, wale wote watakaojihusisha na biashara ya tindikali watalazimika kufikia vigezo vitakavyowekwa," anasema Slim.
Akiongeza, Slim anasema tindikali ni kama kisu. Ni kemikali muhimu kwa matumizi ya kila siku ya mwanadamu, baadhi ikiwa ni kwa matumizi ya betri za magari, dawa za kusafishia vyoo, utengenezaji sabuni na pia kwa matumizi ya mbolea.
Hata hivyo, ikitumiwa vibaya huleta madhara makubwa kwa jamii kwani ina sifa ya kuunguza, kupenya ndani ya mwili na kusababisha vidonda vikubwa, upofu na hata kuua.
"Kisu ni muhimu, lakini kikitumiwa vibaya pia hudhuru. Tindikali iko hivyo pia. Hawa wanaoitumia kudhuru watu wanaitumia kwa nia mbaya... cha msingi ni kuangalia chanzo cha matukio haya na kuwabaini wahusika ili wachukuliwe hatua," anasema Mkemia Slim.
Vinginevyo, Slim anasema kuna hatari kuwa hata jitihada zinazoendelea kufanywa katika kudhibiti biashara holela ya tindikali zikakosa maana ikiwa wahalifu wataendelea kuwapo kwani wanaweza kuendelea kudhuru watu kwa kutumia silaha nyingine kama bastola na hata maji ya moto.
Anasema kuwa kwa hali ilivyo sasa, inaonekana kuwa kwa wahalifu, tindikali ni mbadala wa silaha nyingine kwa vile inapatikana kirahisi. Na kwamba sasa kuna haja ya kuwabaini wahalifu kwani wakiachwa bila kuchukuliwa hatua za kisheria, wanaweza pia kutumia silaha nyingine na kuendelea kutimiza dhamira zao ovu za kudhuru watu.
"Hata maji ya moto yanaweza kutumiwa vibaya na wahalifu kwa nia ya kuumiza watu wasiokuwa na hatia. Tuendelee na harakati za kudhibiti upatikanaji wa tindikali, lakini pia tushirikiane vya kutosha katika kusaka kiini cha matatizo haya," anasema Mkemia Slim. itaendelea kesho.

chanzo:nipashe
No comments:
Post a Comment