Wednesday, 11 September 2013

Madee na Jebby wazitwanga Fiesta Iringa

                                                              Madee
                                                         Jebby

WASANII wenye majina makubwa katika tasnia ya Bongo fleva, Ahmad Ally ‘Madeena Jenebi Mbaraka ‘JebbyJumapili walitia doa tamasha la Serengeti Fiesta baada ya kuzusha vurugu nyuma ya jukwaa, kwenye Uwanja wa Samora mjini hapa.
Katika vurugu hizo zilizochukua takriban dakika tatu, ziliweza kumalizwa kwa ushirikiano mkubwa na busara za Juma Nature, Chege, Mh. Temba na Ruge Mutahaba.
Madee anayetamba na wimbo wa ‘Nani Kamwaga Pombe Yangu na Jebby aliyetamba na ngoma zake kama ‘Swahiba', Tanzania Daima ilishuhudia Jebby akivuja damu mdomoni baada ya kupigwa kichwa na fulana aliyovaa kubaki na damu zilizovuja, hadi mwandishi wa habari hizi alipotoa shati lake kuweza kumsitiri msanii huyo kutokana na baridi kali iliyokuwa uwanjani hapo.
Ukiondoa dosari hiyo, tamasha hilo lilishuhudiwa na umati wa wapenda burudani mkoani Iringa, ambapo lilianza majira ya saa kumi jioni kwa wasanii chipukizi wa mjini hapa kupanda jukwaani na kutoa burudani kali.
Ilipofika majira ya saa 4 usiku, mshindi wa EBBS 2012, Walter Chilambo, alikuwa wa kwanza kushambulia jukwaa kwa vibao vyake vya ‘Siachina ‘Dorovilivyopokewa vema na mashabiki, ikiwa ni mara ya kwanza kupanda katika Mkoa wa Iringa.
Msanii aliyefuatia alikuwa chipukizi wa kike aliyefanya vizuri na kisha jukwaa likavamiwa na Rich Mavoko na ngoma zake za ‘Marry Mena ‘One Timeambazo idadi kubwa ya mashabiki walijitokeza kumpa shangwe za nguvu baada ya kupiga bonge la shoo.
Msanii ‘tajiri wa mahabakama anavyopenda kujiita, Kasimu Mganga, alifanya vema na ngoma yake ya ‘I love Youna kisha kupokewa na mwanadada kutoka THT, Linna aliyepgawisha na nyimbo zake za ‘Chukina ‘Mtima Wange, akafuata Shilole aliyetesa kwa mauno yake.
Ulipowadia muda wa Hip Hop, aliyekuwa wa kwanza alikuwa ni ‘Rais wa Manzese, Madee aliyeimba ngoma yake ya ‘Nani Kamwaga Pombe Yanguna kupokewa na shangwe za kutosha.
Juma Nature alikuwa msanii wa mwisho na kama ilivyo kawaida ya mashabiki wa Iringa wanavyompenda, waliimba naye mwanzo hadi mwisho.
Wasanii wengine waliofanya vizuri ni pamoja na Ney wa Mitego, Stamina, Young Killer, Chege, Mh. Temba, Nick wa Pili, Ney wa Mitego na Ommy Dimpoz.
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment