Monday, 30 September 2013

Ujasusi hautajwi hadharani yasema Kenya

Waziri Joseph Ole Lenku alilitoa maanani swala hilo la mwandishi wa BBC na kusema kuwa taarifa za ujasusi, yaani intelijensi, ni swala la serikali:
"Sifikiri kama weye ndie wa kuniambia mimi nini serikali ingefaa kusema au la.
Kuhusu taarifa na ujasusi wetu, hilo halijakuhusu.
Tumeonesha hapa, na tunaendelea kusema, kuwa taarifa za ujasusi zitabaki hivohivo, habari za ujasusi; na hatutasema hadharani.
Kwa hivo intelijensia yetu ni siri na siyo kitu tutakizungumza hadharani."
Waziri huyo wa Kenya piya alizilaumu nchi, pamoja na Marekani, ambazo zimeonya wananchi wao wasiende Kenya.
Alisema ilani kama hizo hazihitajiki na wala si za kirafiki na hazisaidii katika kupambana na ugaidi wa kimataifa.
Alisema Kenya haitawaachia magaidi kuwatia khofu watu wa Kenya.
chanzo:bbc

No comments:

Post a Comment