Wednesday, 4 September 2013

Ujio mpya wa ‘Ray C’

MASHABIKI wa msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini ambaye anatajwa kuwa ni bingwa kunyonga kiuno, Rehema Chalamila ‘Ray C’, wameanza kujiwinda kusubiri ujio wake mpya ikiwa ni baada ya kupitia katika misukosuko mikubwa ya kimaisha iliyomsababishia kuingia kwenye utumiaji wa dawa za kulevya.
Mkali huyo ambaye utumiaji wake wa dawa za kulevya ulimlazimu Rais Jakaya Kikwete kuwa miongoni mwa wadau waliojitokeza kumsaidia aweze kuachana na hali hiyo tayari ameanika mkakati wake wa kuachia kazi mpya hivi karibuni baada ya kimya cha muda mrefu tangu akumbwe na sakata hilo.
Kwa nyakati tofauti baadhi ya wadau wa muziki na mashabiki wa Ray C wameeleza kuwa kipaji alichonacho mwanamuziki huyo kinaweza kumrudishia makali yake aliyokuwa nayo iwapo atajipanga sawasawa.
Ray C alieleza kuwa kwa sasa anaendelea na matibabu lakini mara atakapomaliza kliniki hiyo maalumu ataachia wimbo mpya ambao anaamini mashabiki na wadau wake wataupokea kwa mikono miwili kuonyesha kukubali ujio wake

No comments:

Post a Comment