Utafiti huo unaonya kuwa nchi nyingi duniani, hazina mifumo mizuri ya kutunza wazee.
Ifikapo mwaka 2050, wazee watakuwa wengi kuliko vijana walio chini ya miaka 15, wengi wakiwa ktika nchi zinazostawi.
Utafiti huo ulikusanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kukadiria idadi ya watu, UNPF na shirika la kimataifa la kutetea maslahi ya wazee HelpAge.
Watafiti wanasema walitumia vigezo 13 ikiwemo mapato, ajira, huduma za afya, Elimu, na mazingira....katika kile wanachosema ni utafiti wa kwanza wa aina yake duniani.
Aidha , watafiti wanasema kuwa nchi nyingi kote duniani zinakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na idadi kubwa na inayoendelea kukuwa ya wazee 72katika mataifa hayo.
"kutokana na ongezeko la mahitaji ya nchi mbali mbali duniani, nchi hizi nazo zinaendelea kukabiliwa na matatizo ya kukidhi mahitaji ya wazee,'' alisema Silvia Stefanoni, kaimu afisaa mkuu mtendaji wa shirika la HelpAge International.
Sweden ilikuwa ya kwanza katika nchi bora zaidi kwa kukidhi mahijati ya wazee, Afghanistan ilikuwa ya mwisho. Mataifa ya ulaya ndio yalifanya vyema katika kuwatunza wazee.
Sio kwa kuwa nchi hizo ni tajiri ndiposa zinawatunza wazee vyema kwa sababu hata nchi ambazo uchumi wao sio mzuri, bado huwatunza vyema wazee, ikiwemo Sri Lanka, Bolivia na Mauritius.
Urusi ilikuwa nambari, (78), India (73) na Uturuki (70) wakati Brazil ilishikilia nambari (31) huku China ikiwa nambari (35)
No comments:
Post a Comment