Wednesday 6 November 2013

M23 'wamaliza uasi' baada ya kipigo

 
Katika taarifa walioitoa waasi hao wamesema badala ya kufanya uasi sasa wataendesha harakati zao kutumia njia ya kisiasa.
Muda mfupi uliopita Kiongozi wa waasi hao Bertrand Bisimwa ametangaza kuwaamuru mkuu wa wapiganaji wa M23 na makamanda wa vikosi vyote muhimu wa kundi hilo kuwaandaa wapiganaji wao kusalimisha silaha, kutawanyika kuondoka katika eneo la mapigano na kukubaliana na matakwa yatakayowekwa na serikali ya Congo
Awali Msemaji wa Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Lambert Mende aliambia BBC kuwa majeshi ya nchi yameishambulia ngome ya mwisho ya waasi na wamekimbia na wengine huenda wakawa wamejisalimisha.
Majeshi ya serikali ya Kongo yakishirikana na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa kilichopewa uwezo wa kupambana na waasi hao walianza mapambano dhidi ya M23 Octoba mwaka huu na kufanikiwa kuwaondoa katika eneo la Bunagana kwenye mpaka wa Uganda ambayo ni ngome yao muhimu.
chanzo:bbc

No comments:

Post a Comment