Saturday 7 December 2013

Watoto 100 walawitiwa Ilala

WATOTO wa kike 100 wamelawitiwa na kubakwa katika manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, huku wanawake 20 nao wakifanyiwa vitendo hivyo kati ya Aprili hadi Desemba mwaka huu.
Takwimu zinaonyesha kuwa watoto wa kiume 56 na wanaume 10 walilawitiwa katika kipindi hicho huku waliopigwa wakiwa ni watoto 33 na watu wazima 16.
Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Dk. Willy Sangu, alitoa takwimu hizo jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi wa kituo cha ‘One Stop’ katika Hospitali ya Amana ambacho kitakuwa kikitoa matibabu kwa wahanga wa matukio ya ukatili wa kijinisia.
Dk. Sangu alisema katika matukio hayo watoto sita walitelekezwa na watu watano walichomwa moto, vitendo ambavyo vinadaiwa kuongezeka kwa kasi ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Hata hivyo, alisema pamoja na idadi hiyo ni mashauri matatu ndiyo yamefikishwa mahakamani, hali inayochangiwa na watendewa kushindwa kutoa ushirikiano.
Alizitaja sababu za ushirikiano mdogo ni wanaotenda vitendo hivyo kuwa ndugu wa karibu wa wahanga hao na hivyo kuamua kumaliza kesi hizo nyumbani.
Kutokana na hali hiyo, Dk. Sangu alisema kufunguliwa kwa kituo hicho kutakuwa ni mkombozi kwa wahanga hao, kwani mpaka sasa ni watu 257 walioifishwa hospitalini hapo kwa kufanyiwa vitendo hivyo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Juma Bwire, alisema kufunguliwa kwa kituo hicho ni mwendelezo wa Jeshi la Polisi katika kupinga ukatili kwa kinamama na watoto
chanzo:daima

No comments:

Post a Comment