Na kwa wanaume, mfumo huu umewaambia, kwa kadri ya mfumo wa malezi katika jamii zetu, kwa kusimamiwa au kuona na kuiga, kuwa wao ndio wakuu wa familia, wakuu wa nyumba, wakuu wa jamii, watoa ulinzi, watoa mkate na chakula, wenye nguvu kuliko wanawake na watoto, wenye akili nyingi na busara, na wenye utambuzi wa hali ya juu.
Kwa vile ushahidi wanao, basi hawatambui kuwa, kile wanachodhani ni msingi wa ukuu na uongozi wao, ni zao la malezi na sio baraka za Mungu, kuwa aliwataka wawe wenye akili sana na uwezo mkubwa sana katika kila kitu.
Na ukisoma kwenye sayansi ya akili na saikolojia ya binadamu unaona kabisa kuwa, hakuna tofauti ya uumbaji kati ya mwanamke na mwanaume katika ubongo na uwezo kiakili, ila tofauti hiyo hutengenezwa na malezi.
Kwa vile ushahidi wanao, basi hawatambui kuwa, kile wanachodhani ni msingi wa ukuu na uongozi wao, ni zao la malezi na sio baraka za Mungu, kuwa aliwataka wawe wenye akili sana na uwezo mkubwa sana katika kila kitu.
Na ukisoma kwenye sayansi ya akili na saikolojia ya binadamu unaona kabisa kuwa, hakuna tofauti ya uumbaji kati ya mwanamke na mwanaume katika ubongo na uwezo kiakili, ila tofauti hiyo hutengenezwa na malezi.
Mwanaume anajua mengi kuliko mwanamke kwa sababu tu mwanamke haruhusiwi kusoma sana au haruhusiwi kufanyakazi nje ya nyumbani, au kwa sababu malezi yalisema haimpasi yeye kujua mengi, mengine ni ya wanaume tu, kwa sababu kuna mgawanyo wa kijinsia katika kila mwenendo na katika kila jambo, haruhusiwi kusoma vitabu fulani ila kwa ruhusa ya wanaomlea na kumsimamia.
Hatimaye mwanamke anaonekana duni katika hili au lile, na hili hatimaye huonekana ni la kiasili (nature) na sio la kimalezi- (nurture). Tunaanza kusema tumejaaliwa hili na Mungu ila wanawake hawakujaaliwa hilohilo.
Mungu hawezi kufanya hivyo, ila malezi yetu ya kiupendeleo ndio yamewajaalia wanaume na wanawake haiba tofauti.
Lakini wanaume wanadhani ni kufaidi na wanawake wanadhani wanaume wanafaidi, kuwa walinzi na watekelezaji wa mfumo dume.
Mfumo wowote hujenga dhana- mara nyingi ya kimakosa, kuwa wale wote wanaofanana huwa wanafaidi kupitia mfumo huo, au wanapata hasara wale ambao hawakuweka katika daraja la usimamizi.
Wanawake wanawaona wanaume wanafaidi, na wanawake wanajiona wao hawafaidi katika mfumo dume.Mtazamo huu unaweza kuwa kweli lakini kwa kiasi kikubwa sana. Kwanza mfumo huu unajenga msingi ambao wanawake hawawezi kutumia uwezo wao waliojaliwa, kuzaliwa nao, kwa uwezo mkubwa wawezavyo.
Mfumo dume unawakataza kuonyesha kuwa wana akili sana, kuonyesha kuwa wanabusara sana, kuonyesha kuwa wana uwezo wa kupata fedha na kuwa nazo, kuonyesha kuwa wanaweza kusoma na kufaulu masomo.
Hayo yanapaswa kufanywa na kuonyeshwa na wanaume, tukidhania kuwa kila mwanaume kazaliwa na uwezo wa juu wa kuonyesha yote hayo. Wengi wa wanaume wana uwezo wa kawaida tu katika yote hayo, na kuna wanawake wengi ambao wakipewa fursa na kuachwa huru wanaweza kuwashinda wanaume katika hayo yote.
Kwa sababu wanaume wanalazimika, kimfumo, kuonyesha uwezo huo mkubwa ambao wengi hawana, wanajikuta wanateseka sana na kupoteza kujiamini mbele ya wanawake, wawe ni wake zao, dada au wapenzi.
Atataka kuonyesha kuwa ana akili sana, ana uwezo wa kufaulu masomo, uwezo wa kuwa na fedha na mali, uwezo wa kurudi na mkate kila siku nyumbani, akishindwa na ikadhihirika kuwa hawezi, anachanganyikiwa.
Anajitesa kisaikolojia. Hataki kumshirikisha mkewe katika kushindwa huko, akiogopa kuzomewa, kuonekana hafai, kuonekana mjinga mbele ya mke, ambaye yuko tayari kuongeza nguvu, ana uwezo na ujanja, ila tu mfumo unasema subiri kila kitu kifanywe na mume.
Wanaume wanaposhindwa wanakuwa wakali, wagomvi, wenye hasira, na wengine kukosa kujiamini. Na wachache huwa walevi, wagomvi dhidi ya wake zao ili kutaka kuonyesha kuwa bado ni wanaume wale wale wakuu wa kaya ingawa hawawezi kuonyesha uwezo huo.
Na wengine wanajiua wakiona kuwa hawawezi kabisa kuonyesha uanaume wao kikamilifu. Ninachosema kuwa sio kweli kuwa kila mwanaume, na kama sio wanaume wote, anafaidi katika mfumo dume.
Kuna wengi hawafaidi na wengi wanateseka kwa kufanyakazi kubwa kuzidi, kuhangaika kuliko uwezo, kujitutumua kufanya mambo, huku wakijua hawayawezi, wakijua kuwa wake zao wanaweza kuyafanya hayo, lakini mfumo unasema ukimwachia mwanamke na akayafanikisha, utadharaulika.
Kwa ufupi ni kwamba, kwa kutekeleza mfumo dume, wanaume tunakosa fursa ya kufaidi kile kikubwa ambacho wanawake wamejaaliwa katika akili zao, ubunifu wao, katika uwezo wao wa kufanyakazi.
Mfumo dume haumfanyi mwanaume kufaidi, na hakuna mwenye uwezo wa kutimiza matakwa yake yote, awe mwanamke au mwanaume.
chanzo:Nipashe
No comments:
Post a Comment