Thursday 17 July 2014

Afungwa jela miaka 18 kwa kumtumia Obama barua yenye sumu!!

Shannon Richardson, mwenye umri wa miaka 36, kutoka Texas, pia alimtumia meya wa New York Michael Bloomburg barua nyingine iliyokuwa na sumu hiyo hiyo.
Alidai kuwa mumewe waliyeachana naye ndiye alituma barua hizo katika njama ya kumlimbikizia madai hayo.
"sikuwa na nia ya kumdhuru mtu, '' Shannon aliambia mahakama.
Alikiri kosa la kumiliki na kutengeza sumu hiyo mwezi Disemba.
Jaji alimpa hukumu kubwa zaidi ikilinganishwa na kosa lake na pia kutakiwa kulipa faini ya dola 367,000.

Richardson, mama mwenye watoto six, ameigiza katika vipindi kama 'The Vampire Diaries' na 'The Walking Dead.'
Viongozi wa mashitaka wanasema kuwa mwanamke huyo aliagiza bidhaa za kutengeza sumu hiyo kupitia kwa mtandao kisha akatuma barua tatu zilizokuwa zimepakwa sumu hiyo.
Shannon mwenye watoto sita aliomba mahakama kumhurumia kwa kumpa adhabu ndogo
Kulingana na viongozi wa mashitaka, moja ya barua alizomtumia Obama , ilikuwa na maandihsi haya: "kilicho ndani ya barua hii, hakiwezi kulinganishwa na mipango yangu kwako bwana Rais. ''
Barua nyingine iliyopokewa na meya Bloomberg, anayeunga mkono kudhibitiwa kwa bunduki, ilisema, '' mpige risasi mtu yeyote atayekuja kuchukua bunduki za mtu aliyetuma barua hii.''
Barua ya tatu iliyokuwa na kemikali hiyo ya sumu, ilifunguliwa na bwana Mark Glaze, mkurugenzi mkuu wa idara inayofadhiliwa na Meya ya kupambana na silaha haramu.
Richardson katika kumtaka jaji kumhurumia, aliomba msamaha akisema, '' mimi sio mtu mbaya. Sina nia ya kumdhuru mtu yeyote.
Aliomba msamaha na huruma na kusema tayari anahisi ameadhibiwa vya kutosha kwa kunyang'anywa watoto wake sita
chanzo:bbc

No comments:

Post a Comment