Pia alisema kuwa kuendeleza maisha ya Nelson Mandela ilikuwa kumvunjia heshima.
Maoni ya askofu huyo mstaafu wa kanisa la kianglikana, ni sawa na yale aliyetamka Askofu mkuu wa kanisa la 'Canterbury Lord Carey' ambaye pia aliunga mkono usemi huo.
Kanisa la kianglikana limeagiza uchunguzi kuhusu jambo hili.
Akiandika katika jadrida hilo, askofu huyu mstaafu wa kanisa la Anglikana Afrikakusini na mwenye miaka themanini na mbili alisema kwamba ''iwapo twahitaji mashine za kupumua,bila shaka tunahitaji kuuliza ubora wake na vile fedha zinavyotumika.'
'
Vile vile alieleza kuwa ni aibu vile aliyekuwa kiongozi wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliwekwa hai kwa mda mrefu hospitalini katika hatua za mwisho za maisha yake huku akipigwa picha na wanasiasa waliomtembelea.
Amesema kuwa Madiba hakujielewa kwa lolote na tendo lao lilikuwa ukiukaji wa heshima za hayati Mandela.
'Ni kweli kwamba watu watahuzunika iwapo nitasema nisaidiwe kufa lakini kwa kauli yangu binafsi sina shaka na hilo.''
Tutu aliandika kuwa,hata ingawa amebadilisha maoni yake,uhakika wa hapo awali hautiliwi maanani kwenye uhalisia wa mambo yalivyo a hasa kwa wagonjwa walio mahututi.
Sheria kuhusu kusaidia wagonjwa mahututi kufariki nchini Uingereza?
Kulinganaga na sheria ya Bunge ya 1961 inayohusiana na kujiua, ni hatia kuhamasisha au kufadhili mtu kujiua nchini Uingereza na Whales. Yeyote anayekiuka sheria hiyo huweza kufungwa gerezani hadi miaka 14.
Sheria hii inakaribia kufanana ile iliyopo Kaskazini mwa Ireland.
Nchini Scotland kuna utata kwani hakuna sheria maalum inayohusishwa na kujiua, japo kwa maandishi na nadharia mtu huweza kuhukumiwa chini ya sheria zinazohusishwa na kujiua.
Je, Kumekuwepo na jaribio la kubadili sheria hiyo?
Kumekuwa na majaribio kadhaa ya kuhalalisha ufadhili wa wanaotaka kusaidiwa kufariki ,lakini hakuna jitihada iliyofua dafu.
Wanaharakati waliofanya majaribio ya kubadili sheria hiyo walibuni na kugharamia shughuli za tume itakayoshughulikia maswala yanayohusiana na ufadhili wa wanaotka kusaidia kufariki.
Tume hiyo ilitoa kauli kuwa mnamo mwaka 2012 kulikuwa na kesi ngumu ya kuruhusu kufadhili kifo cha wagonjwa mahututi nchini Uingereza na Whales
Hii ni kinuyume na madai yanayotolewa na taaluma ya matibabu, makundi ya kutetea haki za walemavu, na makundi mengine yanayodai kuwa sheria hiyo haifai kubadilishwa ili kulinda vikundi vilivyomo kwenye hatari ya kunyanyaswa na jamii.
Je, hali iko vipi ughaibuni?
Katika nchi zingine kama Ubelgiji, Luxembourg na Uholanzi, sheria zimebuniwa zinazoruhusu kufadhili kifo. Ufaransa inakadiria uwezekano wa kuanzisha sheria kama hiyo, japo kuna upinzani mkali kutoka kwa baraza la maadili ya matibabu nchini humo.
Kundi la makampeni lifahamikalo kama "Dignity in Dying" linatabiri kuwa huenda nchi nyinginezo zikafuata mkondo huo wa kuhalalisha sheria hiyo.
Hata hivyo askofu mkuu wa Canterbury, Justin Welby, anachukulia muswada huo unaohusiana na kufadhili kifo kuwa hatari na kanisa la Uingereza linataka swala hilo kupelelezwa.
Kanisa hilo lilisema tume ya kifalme izingatie maoni ya kitaalamu na kukadiria kwa makini madai tofauti. Kanisa linaamini kuwa muswada uliopo sasa unafaa kutupiliwa mbali na kutoa nafasi ili upelelezi kufanywa.
Watu 110 wanameandikishwa kuzungumza siku ya Ijumaa, muswada huo utakapojadiliwa.
Askofu mkuu Desmond Tutu ametoa mwelekeo kuwa mjadala huo utafanyika siku ya kuadhimisha kifo cha Mandela, siku ambayo hayati Mandela angefikisha miaka 96.
chanzo:bbc
No comments:
Post a Comment