Mwanamuziki ambaye ni zao la Jumba la Vipaji Tanzania ‘THT’ Estalina Sanga ‘Linah’ ameaga rasmi jumba hilo ambapo inadaiwa kwa sasa atakuwa chini ya Kampuni ya No Fake Zone ‘NFZ’ inayoendesha shughuli zake nchini Afrika Kusini.
Akizungumza na Ijumaa msemaji wa kampuni hiyo aliyewahi kushiriki Shindano la Big Brother Africa 2003, Abergail Brigette Plaatjies ‘Abby’ alisema wamemchukuwa Linah ili kuendeleza kipaji chake kimataifa.
“THT imemlea vizuri Linah na kumfikisha hapa alipo sasa sisi kama NFZ tumemchukua ili tuweze kumuingiza zaidi kwenye soko la kimataifa na kwa kuanzia tumeanza kumtengenezea video ya wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la Oleh Tembah,” alisema Abby.
chanzo:.globalpublishers
No comments:
Post a Comment