Wednesday 16 July 2014

Mama Diamond aelezea wanawake wanavyojitongozesha kwa mwanae.

MAMA mzazi wa nyota wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ amesema baadhi ya wasichana wanajitongozesha kwa mwanaye kwa kuwa ni mtu maarufu.
Mama Diamond amesema wasichana wamekuwa na tabia ya kutumia hata namba yake ya simu na kutuma picha za utupu kwake na kwa mwanaye.
“Napata shida kwa kweli, wasichana wanajitongozesha kwa kupitia namba yangu ya simu, mtu anakupigia anamuulizia Diamond na wengine ndiyo wanatuma hadi picha za utupu kwa kutumia hii mitandao ya kijamii wenyewe wanasema,” alisema.
chanzo: GL

No comments:

Post a Comment