MWENYEKITI wa Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, amekerwa na alichosema uzushi dhidi yake kwamba ni shoga.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, msanii huyo alisema anachukizwa na kasumba ya baadhi ya watu kufuatilia mambo binafsi ya watu.
“Napenda kuchukua fursa hii kusema machache, kama ‘nitamboa’ mtu naomba samahani.
“Najua binadamu tumezaliwa tofauti sana, kuna wale wanaoogopa dhambi na wengine wanaopenda dhambi.
“Nimepata taarifa humu kwenye mitandao yetu ya kijamii, kwamba kuna binti anaitwa Zainab ananichafua akiniandika mambo ambayo hayana tija kwangu, kwamba mimi shoga, ana uhakika?
“Nimecheka sana kupata hizi taarifa, nataka kuwaambia ndugu zangu kuwa mti wenye matunda ndio upigwao mawe, namkanya mara moja aache kwani naamini anapoteza muda tu, habari hizi sio za kweli kabisa,” alisema.
Msanii huyo mwenye kipaji cha kuigiza sauti za watu wengine hasa maarufu, aliongeza kuwa anamtakia kila la heri kwa jambo alilomtendea na anamuachia Mungu, ila yeye ana mke na watoto, hivyo anajisikia vibaya sana kuzushiwa.
Aliongeza kuwa anajua wanaamua kumchafua baada ya kujionyesha wazi kwenye siasa.
“Watu wananitumia meseji mbaya, eti mimi nimetumwa na viongozi, mara sijui ni shoga, hakuna mambo hayo, nawataka Watanzania wajue hayo ni mambo ya uzushi, sijui hata yametoka wapi,” alisema.
chanzo:tanzania daima
No comments:
Post a Comment