Monday, 26 January 2015

Mtuhumiwa wa wizi wa rediokoli ya kituo cha polisi ajinyonga

Mtuhumiwa wa wizi wa rediokoli ya kituo cha polisi cha Litembo wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma Bosko Ndunguru (40), amefariki akiwa mahabusi na kitanzi shingoni.

Mwili wake ulikuwa unaning’inia  kwenye dari ya  mahabusi kituo cha polisi Mbinga mjini akidaiwa ni baada ya kujinyonga kwa shati alilokuwa amelivaa  hapo awali.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela , alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1.00 asubuhi.

Msikhela alidaiwa mwaka jana Ndunguru anatuhumiwa kuvunja  kituo cha polisi cha Kijiji cha Litembo na kuiba redio koli  ya kituo hicho na kutoroka lakini baadaye alikamatwa.

Alisema kabla ya kujiua ilidaiwa alilalamika kuwa jamaa zake hawampendi  jambo ambalo liliwashangaza mahabusu wenzake.

Alisema polisi kwa kushirikiana na Mganga Hospital ya Wilaya ya Mbinga waliuchunguza mwili wa Ndunguru na kuthibitisha kuwa chanzo cha kifo ni kujinyonga na kwamba na jamaa zake walikabidhiwa mwili huo.
chanzo:nipashe

No comments:

Post a Comment