JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Msingi Luhumbo wilayani hapa, Consolata Tesha (24) kwa tuhuma za kumtupa chooni mtoto wake mchanga muda mfupi baada ya kujifungua.
Mwalimu huyo alikitupa kichanga hicho Mei 15 mwaka huu saa 11 jioni katika Kijiji cha Luhumbo Tinde na kubainika baada ya wananchi waliokuwa wakipita karibu na shule huyo kusikia sauti ya kichanga hicho ikililia kwenye moja ya vyoo vya shule hiyo ndipo walipokwenda kuangalia na kukikuta kitoto hicho.
Kutokana na kitendo hicho, wananchi hao walianza kukibomoa choo hicho na kukitoa kitoto cha kike kikiwa hai na majeraha sehemu za mashavu na uchunguzi wa awali uligundua kwamba kitoto hicho kilitupwa na Mwalimu Consolata ambaye alitiwa mbaroni na sakari polisi, kwa sasa yupo hospitali na kichanga chake kwa matibabu zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa za jeshi hilo, mwalimu huyo alikiri kufanya hivyo kwa madai kwamba kichanga hicho kilidondoka chooni alipokuwa akijisaidia.
No comments:
Post a Comment