Monday, 9 April 2012

KANUMBA ALIKUWA NA MPANGO WA KUMUOA LULU!!!


WAKATI mwili wa msanii nguli wa filamu nchini, Steven Charles Kanumba ukitarajiwa kuzikwa kesho, mengi yamezidi kuibuka kuhusu siri ya uhusianio wake na Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Habari za uhakika kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ya Kanumba, zinasema, wawili hao walipanga kuoana.
Aidha, chanzo hicho cha uhakika, kimedokeza kuwa, sababu ya wawili hao kuficha uhusiano wao wa muda mrefu, ni kuepuka kuvurugwa na wafitini.
Mbali ya wafitini, pia usiri wa wawili hao ni kuepuka jambo hilo kukuzwa na vyombo vya habari, kitu ambacho walifanikiwa hadi siku ya kifo kilipomchukua Kanumba.
“Unajua wale ni ‘masupa star,’ hivyo stori za uhusiano wao huenda zingeweza kuwapa soko wauza magazeti na kudakwa na wasiopenda maendeleo ya wengine, si unajua tena,” kilisema chanzo hicho.
“Ili kuepusha yote hayo, wao wakaona uhusiano wao waufanye uwe siri ambapo hata wasanii wengi walikuwa hawalijui hilo.” 
Chanzo hicho kiliongeza kuwa, hata kitendo cha Lulu kupitiliza chumbani muda mfupi kabla ya mauti ya Kanumba, ni uthibitisho mwingine wa jambo hilo. 
Hata hivyo, wakati mapenzi ya wawili hao kuwa siri, jambo hilo liliwahi kuripotiwa mara kadhaa na vyombo vya habari.
Hivi karibuni, kulikuwa na madai kuwa Lulu yu mjamzito, lakini si ujauzito wa Kanumba, bali wa kigogo mmoja.
Lulu aliwahi kuhojiwa kuhusu jambo hilo katika kipindi cha Mikasi kinachorushwa na EATV, lakini akikana na kuongeza kuwa, hana hata rafiki wa kiume kutokana na umri wake wa miaka 18.
Aidha, Lulu aliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano na Ray ambaye ni rafiki wa karibu wa Kanumba. 
Hata hivyo, wakati hayo yakiendelea, wengi wa mashabiki wa filamu wamebaki kwenye njia panda wasijue ukweli halisi wa suala hili.

No comments:

Post a Comment