Monday, 9 April 2012

MAGARI: KANUMBA ALIAGA!!!!!


MSANII mahiri wa filamu na maigizo nchini, Charles Magari, maarufu kama ‘Mzee Magari’ amesema kifo cha msanii mwenzake, Steven Kanumba kimemshtua na hataweza kusahau kwa haraka. 
Alisema siku mbili kabla ya kifo cha Kanumba, msanii huyo alimpigia simu saa sita usiku, akisema hilo si jambo la kawaida kwake.
Alisema, baada ya kupokea simu, alimuuliza kama kuna tatizo, lakini Kanumba alimweleza alikuwa akimjulia hali tu.
Kwangu ni kama alikuwa akiniaga, kwa maana si kawaida yake kunipigia simu usiku na kuniamkia tu, nikawa ninajua kuna jambo anataka kuniambia ila sasa amekwenda na jambo hilo hajaniambia,” alisema Mzee Magari.
Mwili wa Kanumba, utaagwa kesho Jumanne kwenye viwanja vya Leaders kuanzia saa 3 asubuhi kabla ya kuzikwa kwenye makaburi ya Kinondoni.
Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, leo anatarajiwa kufika katika msiba huo kutoa pole kwa wafiwa.

No comments:

Post a Comment