Friday, 21 September 2012

IJUMAA SEXIEST GIRL 2011/2012 JACK WOLPER AREJESHWA

HUKU mtifuano ukiwa  mkali kati ya Wema Sepetu na Agnes Masogange, wadau wengi wameomba msanii Jacqueline Wolper arejeshwe kwenye shindano hilo ili mshindi apatikane kutokea tatu bora.
Baadhi ya wasomaji wanaofuatilia kwa karibu shindano hili walisema, mshindi kati ya Wema na Agnes anaweza kupatikana lakini itanoga zaidi Wolper akarudi ili apatikane mshindi namba moja, mbili na tatu.
Kufuatia ombi hilo, sisi hatuna hiyana na tumeamua kumrejesha msanii hyo ambaye naye anaonekana kukubalika kwa wengi, kwani hata kutolewa kwake awali kulikuwa kwa mbinde sana.
Kufuatia hatua hiyo, sasa wasomaji watatakiwa kumpigia kura mrembo anayestahili kuibuka mshindi kati ya washiriki hao watatu. Ili kupiga kura, andika jina la mrembo anayestahili kushinda kisha litume kwenda namba 0786799120.
chanzo:http://www.globalpublishers.info

No comments:

Post a Comment