Tuesday 6 November 2012

Mkutano wa Umoja wa watanzania Ujerumani na Worldmission Sunday Mainaschaff Wafana sana Wahisani washawishika zaidi kusaidia miradi Tanzania !









Watanzania wajumuika kwa wingi katika mkutano wa Worldmission Sunday uliofanyika jumapili ya tarehe 28.10.12. watanzania hao ambao walitoka pande mbali mbali za ujerumani, walihudhuria mkutano huo ambao ulianza  saa nne asubuhi mpaka saa 6 za mchana.  baada ya chakula cha mchana mkutano huo uliendelea  hadi saa 12 za jioni.

Dr, Isak Majura alitambulisha Taifa la Tanzania kwa kuonyesha Presentation ambayo ilitayarishwa na Jumuiya ya Watanzania Ujerumani (UTU)

Vile vile Katibu wa U T U  alionyesha Presentation  ya mradi wa shule ya msingi  ya iliyopo maeneo ya Kigamboni  Dar Es Salaam. ambapo wafadhili kadhaa walionyesha kushawishika sana na kutaka kujua ni jinsi gani wanaweza kuifikia shule hiyo ili kuangalia uwezekano wa kuchangia chochote katika maendeleo ya shule hiyo.

Mara baada ya kukamilika kwa presentation hizo Mgeni Rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini ujerumani Bw. Ali Siwa allitoa salam Rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania  na kuwashukuru watayarishaji wa Mkutano huo kwa upendo na mualiko kwa Umoja wa Watanzania Ujerumani.

Wakati huo huo Bi Tabia Mwanjelwa, (Muimbaji wa Maquiz wa Zamani) aliburudisha kwa kuimba na kupiga gitaa, ambapo aliwaacha hoi wafadhili waliohudhuria katika mkutano huo, Bi Tabia Mwanjelwa alisema sauti yake na utaalamu wake wa kupiga Gitaa ndio mchango wake kwa Watanzania.

Watayarishaji wa  Mkutano huo wamefurahishwa na wameridhika sana na mahudhurio ya Watanzania, pamoja na presentation zote mbili,  na kuahidi kuwa Umoja wa watanzania Ujerumani watapata mialiko mara kwa  mara kunapotokea hafla za aina hii.

Umoja ni Nguvu !
kamati.utu@googlemail.com

No comments:

Post a Comment