Friday 11 October 2013

Abiria atishia kuishtaki Fastjet

Kampuni ya Ndege ya Fastjet imedaiwa kukiuka agizo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) ya kutakiwa kukutana na mfanyabiashara Majaliwa Mbasa kumaliza mgogoro uliopo kufuatia kampuni hiyo kushindwa kumsafirisha kutoka Dar es Salaam  kwenda Johannesburg, Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa barua ya TCCAA yenye kumbukumbu namba TCAA/0.10/350/139 iliyoandikwa Oktoba 2 mwaka huu na kusainiwa na James Mabala kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Fastjet, mamlaka hiyo iliagiza kampuni hiyo kukutana na mfanyabiashara huyo ndani ya siku saba ili kuyapatia ufumbuzi malalamiko yake.

Hata hivyo, Mbasa hadi kufikia juzi  siku saba ilizotoa TCAA zikiwa zimeisha kampuni ya Fastjet ilikuwa haijamwita wala wakili wake kampuni ya Legal Clinics Advocate.

Mmoja wa viongozi wandamizi wa kampinu ya Fastjet, Brown Francsi,  alipoulizwa alisema halifahamu.

Mbasa alisema alikata tiketi Septemba 23, mwaka huu kwa ajili ya kwenda Johannesburg na asafiri na ndege ya kampuni ya Fastjet Septemba 27, mwaka huu.
Alisema Septemba 26, alipigiwa simu kuwa safari imeahirishwa na hivyo kutakiwa akachukue fedha alizotoa kama nauli ambazo ni Sh. 521,560.

Alisema kutoka na usumbufu alioupata alilazimika kuwasilisha dai la kurejeshewa fedha zake pamoja na fidia kutokana na kampuni hiyo kufuta safari ghafla.

No comments:

Post a Comment