Friday 11 October 2013

SWALI LA LEO: Kama magereza ni mafunzo mbona wanaotoka jela hufungwa tena?


Taarifa za kusikitisha ni kwamba wengi wa wale wanaotoka jela, ndio wanaofungwa tena, hivyo kuvusha maswali kama ni kweli magereza ni eneo la kufundisha watu mambo mema au mabaya.
 Kama wanaotoka jela, baadhi yao wanarudishwa tena gerezani kwa kufanya mabaya, tatizo ni nini; uongozi mbovu wa magereza, maofisa magereza wasio na ujuzi au wafungwa wenyewe ndio tatizo?
Idadi ya wafungwa wanaofungwa tena baada ya kumaliza vifungo vyao kutokana na kufanya tena makosa ni wastani wa asilimia 25 ya wafungwa,  hivyo kusababisha hofu miongoni mwa jamii kama ni kweli  magereza ni eneo la kubadilisha watu kuwa bora au kuwatengeneza wawe wabaya wanaporudi katika jamii

No comments:

Post a Comment