Friday 11 October 2013

Rais Kikwete amlilia msanii Bongomovie.

Msanii huyo alifariki juzi katika hospitali ya mkoa waArusha alipokuwa amelazwa akiugua na kuzikwa jana mchana nyumbani kwao katika kijiji cha Enzi wilayani Muheza mkoani Tanga.

Maelfu ya wananchi wa wilaya ya Muheza walifurika katika msiba huo huku vilio vikitawala katika msiba huo mkubwa.

Akisoma taarifa kuhusiana na maandalizi ya mazishi hayo ndugu wa marehemu, Saidi Kimnda alisema kuwa Rais Kikwete ametoa usafiri wa kuwaleta waombolezaji kutoka Arusha mpaka kijiji cha Enzi wilayani Muheza kushiriki mazishi.

Wakati wa uhai wake, msanii huyo alirekodi filamu tatu ikiwamo iitwayo "Jesca" na pia alifanya kazi nyingine katika maeneo mbalimbali na uigizaji.

Mazishi hayo ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali, yaliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, Balozi wa Ujerumani Patric Marmon na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Ummy Mwalimu.


Wengine ni Mjumbe wa NEC-CCM Wilaya ya Bagamoyo, Riziwani Kikwete, Mkuu wa Usalama Mkoa waKilimanjaro, Selemani Mombo, Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Muheza Makame Seif, Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais ambae hakufahamika jina lake mara moja na wakuu wa wilaya za mkoa wa Tanga.

Akishukuru, kaka wa marehemu Omari Mhando alisema kuwa anamshukuru sana Rais Jakaya Kikwete na viongozi wengine kwa kutoa mchango wao mkubwa katika mazishi ya msanii huyo wa filamu. 

Katika mazishi hayo maelfu ya wananchi wilayani Muheza walifurika huku zaidi ya magari 100 yakiwa yameleta watu katika mazishi hayo kutoka mikoa mbalimbal
Chanzo:nipashe

No comments:

Post a Comment