Friday 11 October 2013

P-Square kutumbuiza Dar Nov.23

Wasanii mapacha kutoka nchini Nigeria, Peter na Paul Okoye maarufu P-Square, wanatarajiwa kufanya onyesho moja nchini Novemba 23 mwaka huu katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, msemaji wa waandaaji wa onyesho hilo, Hillary Daud ‘Zembwela’ wa EATV na EA Radio, alisema wasanii hao ambao wanatamba na kibao ‘Personally’, wataongozana na wasanii wengine 13 kwa ajili ya onyesho hilo.

“Onyesho hilo walitalifanya ‘live’ jukwaani siku hiyo, huku wasanii watakaoongozana nao wakifanya hivyo…lakini watakuwapo wasanii wa hapa nyumbani watakaojumuika na mapacha hao na watafahamika baadaye,” Zembwela.

Zembwela alisema onyesho hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya huduma za simu ya Vodacom na kwamba mashabiki watarajie kupata burudani tosha huku fursa pekee ikiwa kwa wasanii wa hapa nyumbani kujifunza kutoka kwa vijana hao wanaotambulika pia Ulaya na Marekani.

Alisema wasanii wanatakiwa kujifunza mengi kutoka kwa wasanii wanaokubalika kimataifa, hivyo kuja kwa mapacha hao pamoja na wale watakaowasindikiza kutasaidia kujifunza mengi.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom ambao ni wadhamini wakuu wa onyesho hilo, Kelvin Twissa, alisema kampuni yao inafurahia kuwa sehemu ya kutoa burudani kwa jamii ya Watanzania.

Twissa alisema wasanii hao ambao wanakubalika nchini kutokana na vibao vyao mbalimbali, ujio wao utawasaidia wasanii wa nyumbani kujifunza mengi toka kwao.
“Tumekuwa chaguo la kwanza hususani kupitia masuala ya burudani na huduma nyingine za mawasiliano na kijamii…tutaendelea kuunga mkono jitihada za wasanii wetu wa ndani kwa kuwapatia fursa ya kujifunza toka kwa wenzao waliofanikiwa kimataifa,” Twissa aliendelea.

"Kwa wateja wa Vodacom ambao pia ni mashabiki wa wasanii hawa ambao wanatamba na kibao chao kitamu cha ‘Personally’ kwa sasa wanayo fursa ya kufurahia nyimbo hizi kwa 'kuzidownload' au kuzitumia kama miito ya simu (RBT) na kuweza kujishindia tiketi za onesho hilo. Natoa wito kwa Watanzania wapenda burudani kutembelea ukurasa wetu wa Facebook na Twitter kwa taarifa zaidi na kujua namna ya kujishindia tiketi za onesho hilo."

Aidha, alisema onyesho hilo linaloratibiwa na EATV na Radio, na kudhaminiwa na Vodacom, linatarajiwa kuwa la kihistoria kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, kwani ni mara ya pili kwa P-Square kuja
 
 
chanzo:nipashe

No comments:

Post a Comment