Thursday, 16 June 2011

BAJETI YA SERIKALI NA VYAMA VYA UPINZANI.




WAFUTA POSHO, WATANGAZA KIMA CHA CHINI SH 315,000
KAMBI ya Upinzani Bungeni imetangaza bajeti mbadala ya Sh14 trilioni na kubainisha upungufu mkubwa katika Bajeti ya Serikali, huku ikipendekeza kufutwa kwa misamaha ya kodi kwa kampuni za uchimbaji wa madini na mafuta na posho za vikao kwa watumishi wa umma, wakiwamo wabunge.Akiwasilisha bajeti hiyo bungeni, mjini hapa jana, Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe alisema hatua hiyo imelenga kuongeza mapato ya Serikali na kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.

No comments:

Post a Comment