MUIGIZAJI wa siku nyingi katika kundi la Msanii Afrika, Abdul Maisala maarufu kama Maisala anatarajiwa kutoka na filamu yake inayokwenda kwa jina la ‘Chungu’ ambapo ndani yake ataonekana msanii nguli nchini Suzane Lewis ‘Natasha’.
Filamu hiyo ambayo imetayarishwa na Shule & Company imerekodiwa mjini Tanga katika Wilaya ya Lushoto katika Jimbo la Bumbuli.
Maisala alisema lengo la kurekodi filamu hiyo katika mji huo ni katika kuzitangaza maliasili za maeneo hayo yaani utalii wa ndani sambamba na mandhari nzuri na tofauti ambayo haijazoeleka kuonekana katika filamu nyingine.
“Pamoja na hilo pia filamu hii ya Chungu inaelezea mila za kabila la Wasambaa…katika kuleta uhalisia ilitupasa kuchezea filamu hii sehemu kubwa katika wilaya hii na sehemu zilizobaki kuigizwa katika jiji la Tanga. Ni filamu nzuri,” alisema Maisala.
Mbali na Natasha, wasanii wengine walioshiriki ni pamoja na Richard Mshanga ‘Mr. Masinde’, Ali Migomba ‘Wandiba’, Suzane Bila, Suzane Martine, Chacha Nyamakha, Fatuma Titu na wengine.
No comments:
Post a Comment