MKALI wa bongo fleva, Juma Kassim Kiroboto maarufu kama Juma Nature, anatarajiwa kwenda nchini Afrika Kusini kupitia mwaliko aliopewa na familia ya marehemu Brenda Fassie wa huko.
Nature amekula shavu hilo kutokana na kuimba kibao cha ‘Mugambo’ kilichopigwa kwa mtindo wa Kwaito na kutesa sana miaka ya hivi karibuni.
Akiwa huko, Nature atafanya maonyesho matatu katika jiji la Cape Town sambamba na kwenda kuzuru kaburi la Fassie.
No comments:
Post a Comment