Sunday, 12 June 2011

MIRIAM LUKINDO NDANI YA KIRUMBA!!!!!!!

MWANAMUZIKI wa Injili nchini anayefanya vema katika tasnia hiyo, Miriam Lukindo Mauki leo anatarajiwa kuzindua video ya albamu yake ‘Ni Asubuhi’ kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Onyesho hilo la aina yake litapambwa pia na wakali wengine wa muziki huo, wakiwemo Upendo Nkone, Martha Mwaipaja, Joseph Nyuki, Neema Mwaipopo na wengine.
Baada ya uzinduzi huo, Miriam atakwenda Ukerewe ambako Juni 21 atazindua video yake katika Uwanja wa Getrude Mongella.
Albamu hiyo inaundwa na vibao ‘Sema na Moyo Wangu’, ‘Mungu U Mwema’, ‘Wewe ni Sababu’, ‘Anasikia’, ‘Amen Amen’, ‘Twende na Yesu’, ‘Amefanya’ na ‘Ni Asubuhi’ uliobeba jina la albamu. 

No comments:

Post a Comment