Mwanamuziki mwenye vituko hasa kwa mtindo wa kupaka rangi nywele zake, toka nchini Jamaica, Elephant Man amefunika kwenye tamasha la Str8Muzik Beach Party 2011 jijini Dar es salaam kwenye klabu ya Mbalamwezi Beach.
Nyota huyo, mwimbaji wa Dancehall Reggae, Elephant Man ambaye kimataifa hujulikana kama Energy God (Mungu wa Nguvu) alipanda jukwaani saa 4:00 usiku na kutoa shoo ya kufa mtu iliyo wafanya mashabiki kila mmoja kucheze na wengine kumfuatisha alivyo kua ana imba.
Mwisho akielekea kumaliza shoo aliishia kusema “ Africa ni nzuri, Tanzania ni kubwa, kuna wanawake warembo (wadada wa Kitanzania mna lijua hilo). Pia alitambua umaarufu wa Buju Bantoni, anayetumikia kifungo jela nchini Jamaica pamoja na kuimba wimbo uitwao “We are the World” katika aina peke ya “sweet reggae” akihitimisha makamuzi yaliyodumu kwa saa moja na nusu.
No comments:
Post a Comment