Saturday, 2 July 2011

DEBORAH AFANYA SANAA TATU TOFAUTI KWA SIKU!!!!!!!!!!!!!!!!!


MSANII wa maigizo, filamu na mcheza ngoma, Deborah Dikson, amesema kwa siku huwa anafanya mazoezi ya kazi tatu tofauti. Deborah alisema mazoezi hayo kwake yanamsaidia katika kujiweka ‘busy’ na kuepuka mambo mengine ambayo kwa namna moja au nyingine yangeweza kumharibia maisha.
Debora kwa sasa anawika katika kikundi cha maigizo cha Kaole, huku akicheza ngoma katika kikundi cha Machozi Theatre Troup na pia ameshashiriki katika filamu mbalimbali.
kamwe hawezi kuacha kucheza ngoma, kwani ndipo hasa palipomfanya ajulikane na kuwashauri wasanii wengine wa kike kutochagua sanaa za kufanya.
 “Unajua kama msanii unatakiwa ujue walau sanaa zisizopungua tano, lakini wewe unacheza tu filamu au maigizo, eti unajiita msanii mimi sioni kama ni sawa na pia nawasihi wasanii wenzangu wapende kujaribu, sio kubakia kusema hawajui,” alisema. 

No comments:

Post a Comment