Mwanadada Aunt Ezekiel sasa ataanza kuonekana kwenye filamu mbalimbali kwa kasi baada ya kumaliza adhabu yake.
Mmoja ya watu walio karibu na mwigizaji huyo anayetingisha kunako anga ya filamu, alisema kifungo hicho kimeisha mwishoni mwa mwaka jana,
Aunt alilazimika kuwekwa kando na waigizaji wenzake kutokana na utovu wa nidhamu alioufanya.
Japo chanzo hicho hakikutaka kuweka wazi kwamba ni nini hasa alichokosa Aunt hadi kupewa adhabu, aliwataka mashabiki kumsubiri dada huyo ambaye alidai anarudi kwa kasi ya ajabu na hii yote ni kutokana na kuwamis na kuwaonesha wadau kwamba amezaliwa na kipaji hicho na wala si cha kujifunza.
No comments:
Post a Comment