Thursday 20 February 2014

Ajali mbaya mlima Sekenke miili ya watu nne yateketea kwa moto!!!






LORI la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya sekenke mkoani Singida na kuua watuwanne papohapo.
Chanzo cha ajali hiyo ni kufeli breki lori hilo kukamata moto wakati lilipokuwa linashuka milima hiyo. Shuhuda wa ajali hiyo, bwana Julius Chacha alipoongea na Dj Sek Blog amesema kuwa lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.
Akiendelea kuongea, shuhuda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwa kuwa moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea. Watu wanne wamekufa papohapo kutokana na ajali hiyo.  Polisi walikuwa bado hawajafika eneoo la tukio mpaka tunaondoka eneo la tukio.
(Picha na DJ Sek Blog)

No comments:

Post a Comment