Wednesday, 29 February 2012

TULIJIIFUNZA NINI NA BLOG YA ZE-UTAMU(ZE-UCHUNGU).

Ze -utamu (ze-uchungu) ni blog ambayo ilikuwa inaongelea maisha ya watu kwa mtindo wa kuzalilisha ,kashfa na mengineyo.Blog hii iliweza kusababisha machafuko kwenye ndoa za watu,wachumba kuachana pia na tafaruku baina ya marafiki na ndugu na majamaa,mwenye roho ndogo ungeweza hata kujiua kwani watu walikuwa wanaaibishwa na kuonekana dunia nzima, na uchonganishi ulikuwa mstari wa mbele.
Cha kushangaza zaidi ni pale watu jinsi walivyokuwa  wanamsaidia kumpa habari za uchonganishi ,kashfa na kudhalilisha watu, kama watu wasingemsaidia isingefika pale ilipokuwa na hata watu wasingiumia kwa kiasi kile.
SWALI KWA WADAU NANI WA KULAUMIWA ZAIDI, KATI MWENYE BLOG NA WATOA HABARI  HIZO ZA KASHFA,UCHONGANISHI,KUZALILISHA NA MENGINEYO.
DUNIA KUJIFUNZA NA KUELIMISHA  KAZI KWAKO MDAU

No comments:

Post a Comment