Saturday 24 March 2012

SINTA SASA HADI KWA ZITTO KABWE!!!!!!



MLIMBWENDE aliyerudi upya katika uigizaji, Christina Manongi ‘Sinta’, hivi karibuni anatarajiwa kuachia filamu zake mbili kwa mpigo, moja akiwa amewashirikisha wanasoka na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Akizungumza katika kipindi cha Block4teen, Sinta alisema filamu hizo ni ‘Sitaki Demu’ atakayoyocheza na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Juma Nature na nyingine ni ‘Returning of J-LO’ ambayo ndio amewashirikisha wanasoka na Zitto, ambayo itakuwa ikielezea maisha yake hadi kuifikia umaarufu aliokuwa nao kwa sasa.
Aliwataja wachezaji aliowashirikisha katika filamu hiyo kuwa ni Jerryson Tegete wa Yanga, Amir Maftah na Emmanuel Okwi wa Simba.

No comments:

Post a Comment