Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema mwanamume huyo alikufa
juzi saa 5.00 usiku karibu na Hospitali ya Dk. Mvungi.
Alisema kuwa Kitupa akiwa anaendesha gari lenye namba za usajili T 360 NUL aina ya Suzuki
huku akiwa ameongozana na Alluu, alianza kutokwa na povu mdomoni na puani ghafla.
Kutokana na hali hiyo, Kenyela alisema mwanamke huyo aliamua kuliendesha gari hilo hadi katika Hospitali ya Dk. Mvungi na alipofanyiwa uchunguzi aligundulika kwamba alishafariki dunia muda mrefu.
Kenyela alisema chanzo cha kifo hicho ni ugonjwa wa shinikizo la damu ambao ulikuwa ukimsumbua Kitupa kwa muda mrefu na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi. Katika tukio lingine watu sita wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kupatikana na kete 25 za bangi pamoja na lita 24 za pombe haramu ya gongo.
Watuhumiwa hao ambao wametajwa kuwa Safari Mohamed (36), Aman Ally (27) na wenzao wanne walikamatwa juzi katika maeneo ya Kigogo na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma zinazowakabili.
NA HABARI YA LEO
No comments:
Post a Comment