MUIGIZAJI nyota wa filamu nchini, Riyama Ally, amesema nidhamu aliyonayo katika tasnia ya uigizaji, hajioni mpaka leo kuwa yeye ni ‘Super Star’ kuliko waigizaje wengine.
Riyama alisema kwamba ni kutokana na hilo ndiyo maana anaweza kucheza nafasi yoyote na msanii wa aina yoyote yule hata kama ni chipukizi.
“Ukweli ni kwamba wasanii wengi ambao wameshakuwa na majina, wana tabia ya kuwanyanyapaa wasanii wachanga, lakini kwangu hilo ni tofauti kwa kuwa naamini hata mimi nilitokea huko,” alisema Riyama.
habari na sayari
No comments:
Post a Comment