MUIGIZAJI Hemed Suleman ‘PHD’, anasema filamu ya ‘Redcross’ inayotarajiwa kutoka mwezi ujao hataisahau katika maisha yake kutokana na ugumu ambao ameupata wakati wa kuicheza.
Akizungumza na Sayari, Hemed alisema katika nafasi aliyoicheza akiwa kama muhusika mkuu, alikimbizwa sana kitendo kilichomfanya kuvimba miguu kwa sababu hakuwa na mazoezi kwa muda mrefu.
Hata hivyo, PHD ambaye pia ni msanii wa muziki, alisema ‘Redcross’ ni filamu ya aina yake, na ana imani italeta mapinduzi katika tasnia hiyo kutokana na uhalisia uliooneshwa.
habari na sayari
No comments:
Post a Comment