MKE wa mchezaji na mtengenezaji filamu, Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Wastara Sajuki, ambaye pia ni msanii, amesema kuwa ugonjwa unaomsumbua mumewe kwa sasa ulisababishwa na kukaa kwenye kompyuta na kuendesha gari kwa muda mrefu.
Akizungumza katika kipindi cha Leo tena kinachorushwa na Radio Cloud FM, Wastara alisema hilo liligundulika baada ya mumewe kwenda kupata vipimo mara mbili katika hospitali mbili tofauti, ikiwemo Hospitali ya Rufaa Muhimbili.
Dada huyo alibainisha kwamba, Sajuki baada ya vipimo alibainika kuwa ana uvimbe kwenye ubongo, ambao ndio ulikuwa ukimsababishia maumivu ya mgongo na kichwa kwa muda mrefu, ambapo hata hivyo alipatiwa dawa na kuanza kushiriki mazoezi ya viungo jambo ambalo limemsaidia kwa kaisi kikubwa.
habari na sayari
No comments:
Post a Comment